AVM – Kiswahili

Juu ya umoja wa wanaoamini wamisionari wanatakikana kuwa na usikivu

Umoja wa wanaoamini wamisionari kadhaa wanatakikana kuwa na usikivu, unahimiza kutumia mbinu za kuendeleza uinjilisti na maendeleo yanayotegemea rasilmali na lugha za wenyeji. Mambo hayo yanakuwa ya usikivu sababu hayana lengo la kuwalipa wahusika na mali kutoka nje. Kwa hivyo, pasipo wenyeji kusimama na miradi ili ifanyikishwe, mipango ya wageni inaweza anguka kwa rahisi. Mmisionari msikivu, badala ya kujaribu kuiokoa na pesa kutoka nje, atakubali miradi hii ianguke.

Umisionari wa usikivu ni sehemu ya mbinu zinazo jaribu kusaidia watu kuipokea injili katika mazingira yao. Umoja huu unawahimiza wageni wawe wasikivu, ili wafaidike kwa ufahamu unaowajia wanaodhamini rasilmali ya wenyeji na lugha zao. Kwa wanaosema rasilmali hizo zinaonekana na udhaifu, tunasema kama mmisionari wa zamani, “napendezwa na udhaifu … niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu” (2 Wakorintho 12:10).

Lengo Letu

Lengo letu ni kuwahimiza wamisionari kufuata mfano wenye nyenyekevu ya Yesu, aliye kuwa msikivu kwa Wayahudi alipoishi chini ya muktadha wao. Mfano unaochangia kwa usikivu ni ule wa kufanya huduma kulingana na kitamaduni cha wanaofikiwa, kukataa cheo chenye heshima ya juu, kutumia lugha za wenyeji, and kutopendelea utumizi wa rasilmali kutoka nje.

Kujua Zaidi.